Home » , » Chris Brown:nataka kufa baada ya kutoa album yangu.

Chris Brown:nataka kufa baada ya kutoa album yangu.

Written By Unknown on Friday, December 28, 2012 | 8:21 PM

CB-Chris Brown
'Don't work me up hit maker' ambae amekuwa gumzo kwenye media mwaka huu katika maswala mbalimbali ikiwemo mapenzi yanayotatanisha kati yake na warembo wawili Karruache Tran na Rihanna,
ugomvi wake na Drake na mafanikio yake makubwa katika Muziki, alitoa tamko ambalo liliwashtua wengi siku kadhaa kabla ya kusherehekea sikukuu ya Christmas.

Chris Brown aliandika kupitia Instagram ujumbe unaoonesha ana machungu sana na hili game la muziki, na kwamba anataka kuondoka katika sayari hii baada ya kuachia album yake ijayo.
Chris Brown aliandika kupitia instagram, "Baada ya hii album nataka kuondoka katika hii sayari."

"Wasanii wa kweli ni viumbe waliojiweka hatarini!" Baada ya hapo aliendelea na maneno yenye ukakasi na yanayoonesha hasira, "This gimmick age is f*cking corny as f*ck! Be you but f*cking get credit for the work u do. Not becuz someone cosigns who knows absolutely nothing about music and culture!"

Chris Brown ambae album yake ya Fortune ilipendekezwa kushindania tuzo za grammy za 55 katika kipengele cha Best Urban Contemporary Album, anatarajia kuachia album yake mpya mwaka 2013 inayoitwa 'Carpe Diem'.

Wengi wanajiuliza inakuaje, Chris ameamua kujimaliza ama anataka kuihama vipi hii dunia, ama ametumia maneno ya kisanii na hana maana ya moja kwa moja ya kuihama hii sayari yenye oxygen inayomsaidia binadamu kupumua.

Hata hivyo Chris Brown aliifuta message yake muda mfupi baada ya kuipost.
Share this article :

Post a Comment

 
© 2013. Muziki Wetu Tanzania - All Rights Reserved
Developed by Kicbjamii