Home » , , » Deey Classic ndani ya Tunzo za Kili Time Music-Tz

Deey Classic ndani ya Tunzo za Kili Time Music-Tz

Written By Abdulaziz Issa on Friday, April 26, 2013 | 6:29 PM

Deey Classic
Producer wa muziki kutoka Mwanza - Deey Classic amechaguliwa kuingia katika kinyang'anyiro cha kuwana tunzo katika kipengele cha producer anayechipukia.
Soma alichokiandika kutoka katika blog yake hapa.


Nimechaguliwa kuingia katika kuwania tunzo za muziki Tanzania za Kilimanjaro (Kili Time Music Awards) katika kundi la Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka na namba yangu ni BF1 kama mnavyoona katika picha hiyo hapo juu eneo lililozungushiwa msitari mwekundu na lenye maneno D Classic.
Naamini tutakuwa pamoja katika wakati wote. Nashukuru wote waliowezesha kwa namna moja ama nyingine kuweza kufikia hapa sio rahisi kuorodhesha majina yao wote lakini
popote walipo naomba wazipokee shukrani zangu.
Tuendeleeni kupeana moyo na kazi tuzidi kufanya kwa ushirikiano mkubwa.
Kwa yeyote mwenye maoni ama ushauri asisite kuwasiliana nami.
KARIBUNI!

Share this article :

Post a Comment

 
© 2013. Muziki Wetu Tanzania - All Rights Reserved
Developed by Kicbjamii